Kwa ufupi:
PAMBA ni zao ambalo hustawi vizuri sana katika
sehemu kubwa ya nchi yetu. Pamba hustawi katika udongo
wa aina mbali mbali mradi tu maji yawe yanapenya kwa
urahisi na usiwe na chachu (acidic) kwa wingi. Kiasi cha
inchi ishirini za mvua hustawisha pamba vema, kama
ikinyesha kwa mpango mzuri. Mwinuko wa kuanzia usawa
wa bahari hadi futi 4,500 kutoka usawa wa bahari ndiyo
hasa hufaa kwa ustawishaji wa pamba.