Kwa ufupi:
Mpango wa utafiti wa Binadamu na Mazingira Mikoa ya Kati Tanzania unaendeshwa
kwa ushirikiano kati ya Institute of Resource Assessment (IRA), Chuo Kikuu cha Dar es-salaam, nchini Tanzania, na Environment and Development Studies Unit (EDSU),
School of Geography, Stockholm University, Sweden.
Watafiti wapatao kurni na tano kutoka nyanja mbalimbali wanahusika na utafiti huu.
Vyuo hivyo viwili vinashirikiana katika rnipango mbalimbali ya kuandaa na kutekeleza
shughuli za utafiti. Mpango huu unaratibiwa na Mkurugenzi wa IRA, Profesa Idris
Kikula na Mkuu wa kitengo cha EDSU, Profesa Carl Christiansson. Fedha kwa ajili ya
mpango huu zimetolewa na the Swedish Agency for Research Cooperation with the
Developing Countries, SAREC.
Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kutumika na idara mbalimbali za serikali na
mashirika ya umma,miradi ya Hifadhi Ardhi na Mazingira na mashirika mbalimbali ya
kimataifa yaliyo katika rnikoa hiyo. Wakati huo huo matokeo ya utafiti huo yatasaidia
katika kuelewa hali halisi ya mazingira na maturnizi ya ardhi katika rnikoa inayohusika.
Makala haya yana taarifa ya utafiti uliofanyika katika kuchangia mpango huo. Orodha
ya makala mengine yanayohusiana na mpango huo wa utafiti yanapatikana kutoka
Institute of Resource Assessment, Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, S.L.P.35097, Dar es-salaam au kutoka the Environment and Development Studies, School of
Geography, Stockholm University, S-106 91 Stockholm, Sweden.