Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na
Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula (MAFS), pamoja na Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa
Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo
Tanzania.
Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya
Wakulima, Watafiti na Washauri wa Ughani. IIi kufikia lengo hili,
mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana
ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda.
Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara iliyofanyika mwezi Machi
2003. Ziara hii iliwashirikisha wakulima na washauri wa ughani
kutoka Kanda ya Mashariki ikijumuisha wilaya za Handeni, Lushoto,
Morogoro, Bagamoyo, Kibaha, Korogwe na kanda ya Nyanda za Juu
Kusini ikiwajumisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya
za Mbeya Mjini, Njombe, Sumbawanga, Songea, Rujewa, Namtumbo
na Iringa Mjini, ambao walitembelea wakulima wa wilaya ya Njombe,
Iringa. Ripoti hii pia inapatikana katika lugha ya kiingereza.