Kwa ufupi:
Katika nchi za Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini magonjwa
makuu ya mifugo ni yale yanayosababishwa na viini vidogo
vya' chembechembe moja vinavyoitwa Protozoa, ambavyo
husambazwa kwa wanyama na aina mbalimbali za kupe na
ndorobo (mbung'o). Kupe na mbung'o wanaambukizwa na
viini ambavyo vinaambukiza mifugo pia na kusababisha
magonjwa na vifo vingi. Udhibiti wake ni mgumu na wa
qhararna kubwa sana. Kwa sababu ya magonjwa haya, faida
za mifugo katika nchi hizi zitaonekana endapo magonjwa ya
kupe na ndorobo yatatokomezwa. Kijitabu hiki kinaeleza dalili
za ugonjwa wa ndigana kali kwenye ng'ombe, pamoja na zile
za mnyama aliyekufa kwa ugonjwa huu. Walengwa wa elimu
hii ni wafugaji iii, waweze kudhibiti magonjwa ya mifugo
yanayoenezwa na kupe kwenye mifugo yao. Kijitabu
kitawaelimisha na kuwanufaisha pia watafiti, wataalamu,
wanafunzi na maafisa wa Serikali wenye uamuzi kuhusu sheria
na sera za kuendeleza ufugaji Tanzania na nchi zingine za
Afrika. Kijitabu kimetoa maelezo kamili kuhusu maradhi ya
ndigana kali, ugonjwa hatari sana wa ng'ombe una
wanyama wote wanaoambukizwa, kwa sababu mfugaji
akidhibiti ndigana kali atakuwa amedhibiti magonjwa yote ya
kupe.