Kwa ufupi:
Kitabu hiki cha mwongozo wa ufugaji bora wa samaki kimeandaliwa na kuandikwa na watalaamu
wabobezi wa taaluma ya ufugaji wa samaki toka Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Morogoro.
Kimeandaaliwa ili kuchangia katika kukidhi mahitaji ya
kitaalamu kwa wafugaji wa samaki aina ya perege au sato,
kwa vile utafiti umebaini kwamba katika miaka ya hivi
karibuni watu wengi wameanza kufuga samaki bila ya
kuwa na elimu sahihi. Kitabu hiki cha mwongozo kimeeleza
mambo yote ya msingi kwa ujumla wake kuanzia kuchagua
eneo la mradi hadi uvunaji na uuzaji wa samaki aina ya
perege au sato