Kwa ufupi:
Carnation’ ni ua ambalo asili yake ni nchi za Ulaya zenye hali ya hewa ya baridi. Hapa Tanzania maua ya ‘carnation’ yaliletwa na wazungu katika vipindi tofauti. Mpaka sasa maua haya yanalimwa vijiji vya Tchenzcma na Nyandira huko Mgeta na kijiji cha Ruvuma (Morning Side) mkoani Morogoro. Maua aina ya ‘carnation’ pia yanalimwa na kampuni ya Highlanders wilayani Njombe na kijiji
cha Ndiwili wilayani Kilolo katika mkoa wa Iringa. Mpaka sasa ugavi wa maua ya ‘carnation’ hautoshelczi mahitaji ya soko la ndani. Kwa mfano, wafanyabiashara wanahitaji zaidi ya banchi 100,000 kwa mwaka wakati wakulima hawawezi hata
kuzalisha nusu yake. Matokco yakc maua mengi ya ‘carnation’ kwa ajili ya soko la ndani hununuliwa toka Nairobi nchini Kenya. Ni dhahiri kuwa watu wengi nchini Tanzania hawajui kiliino cha maua ya ‘carnation’. Sehemu hii ya kijitabu ina lengo la kuelezea juu ya kilimo cha ‘carnation’ kwa wakulima wadogo wadogo. hasa uzalishaji wa michc, upandaji wa michc bustanini, utunzaji wa
bustani na uvunaji wa maua.