Kwa ufupi:
Warsha iliandaliwa na Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la
Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania (TARP II SUA)
unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoinc cha Kilimo (SUA) kwa
kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula pamoja na Chuo
Kikuu cha Norway cha Kilimo (NLH). Lcngo kuu la warsha lilikuwa ni kubaini sababu zinazofanya uzalishaji wa kuku wa kienyeji kutokidhi mahitaji ya soko na kubuni mbinu za kukabiliana nazo ili mkulima aweze kuongeza uzalishaji wa kuku wa kienyeji na anufaike na soko lililopo la kuku wa kienyeji. Warsha ilikuwa na madhumuni mahsusi yafuatayo ili kufanikisha lengo hilo.