xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.contributor.author Inades formation Tanzania
dc.date.accessioned 2024-05-06T07:57:35Z
dc.date.available 2024-05-06T07:57:35Z
dc.date.issued 1992
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/870
dc.description Jarida en_US
dc.description.abstract Tanzania ina idadi kubwa ya kuku wa kienyeji wanaofugwa kwa mtindo wa huria vijijini na hata mijini. Katika mtindo huu wa ufugaji, kuku huachwa huru mchana kutwa kujitafutia chakula wao wenyewe. Pengine baadhi ya wakulima huwatupia kuku wao mabaki ya chakula, chenga za nafaka au nafaka zenyewe. Wapo pia wakulima walio na utaratibu wa kuwapa kuku wao pumba za nafaka na maji ya kunywa kila inapowezekana. Zinapofika nyakati za jioni kuku hulala jikoni, au ndani ya nyumba ya mkulima mwenyewe. Ingawaje ufugaji wa aina hii ni rahisi, lakini faida inayopaikana (kama ipo) ni ndogo sana. Kutokana na kuzaana wenyewe wa wenyewe (kutobadili jogoo), lishe duni n.k., kuku hawa wana umbo dogo. Hutaga mayai machache, tena madogo madogo. Nyama yao ina ladha nzuri, lakini kwa vile wana umbo dogo, kiasi cha nyama wanayotoa ni kidogo tu. Katika kijitabu hiki “Kufuga na Kuboresha Kuku wa Kienyeji” tutazungumzia jinsi ya kuboresha kuku wa kienyeji kwa njia ya uzalishaji, kutumia jogoo bora, kuboresha lishe ya kuku. Tutazungumzia pia njia mbalimbali za kufuga zinazoweza kumnufaisha mfugaji mdogo. Kutokana na maarifa haya wewe mkulima utaweza kuona haja ya kufanya mabadiliko katika ufugaji wako. Hi uweze kunufaika na ufugaji ni lazima uwe na mifugo bora. Kitabu hiki kimeandikwa ili kukupatia maarifa na mbinu za kutumia ili upate kuku bora kutokana na kuku wako wa kienyeji. Katika kitabu kingine “ Kufuga kuku wa biashara” Utajifunza maarifa na mbinu bora za ufugaji wa kuku wa biashara. Hawa ni kuku wa kigeni. Wanahitaji matunzo maalum tofauti na yale ya kuku wa kienyeji wanaoboreshwa. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher inades formation Tanzania en_US
dc.subject Kuku en_US
dc.subject Ufugaji en_US
dc.subject Kuku wakienyeji en_US
dc.subject Mafunzo ya Ufugaji en_US
dc.title Mafunzo ya ufugaji en_US
dc.title.alternative ;kufuga na kuboresha kuku wa kienyeji. en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu