Kwa ufupi:
Tanzania ina idadi kubwa ya kuku wa kienyeji wanaofugwa kwa mtindo wa huria
vijijini na hata mijini.
Katika mtindo huu wa ufugaji,
kuku huachwa huru mchana kutwa kujitafutia chakula wao wenyewe.
Pengine baadhi ya wakulima
huwatupia kuku wao mabaki ya chakula,
chenga za nafaka au nafaka zenyewe. Wapo pia wakulima walio na utaratibu wa kuwapa kuku wao
pumba za nafaka na maji ya kunywa kila inapowezekana.
Zinapofika nyakati za jioni
kuku hulala jikoni,
au ndani ya nyumba ya mkulima mwenyewe. Ingawaje ufugaji wa aina hii ni rahisi, lakini faida inayopaikana
(kama ipo) ni ndogo sana.
Kutokana na kuzaana wenyewe wa wenyewe (kutobadili jogoo),
lishe duni n.k.,
kuku hawa wana umbo dogo.
Hutaga mayai machache, tena madogo madogo. Nyama yao ina ladha nzuri,
lakini kwa vile wana umbo dogo,
kiasi cha nyama wanayotoa ni kidogo tu.
Katika kijitabu hiki
“Kufuga na Kuboresha Kuku wa Kienyeji”
tutazungumzia jinsi ya kuboresha kuku wa kienyeji kwa njia ya uzalishaji,
kutumia jogoo bora, kuboresha lishe ya kuku.
Tutazungumzia pia njia mbalimbali za kufuga zinazoweza kumnufaisha mfugaji mdogo.
Kutokana na maarifa haya
wewe mkulima utaweza kuona haja
ya kufanya mabadiliko katika ufugaji wako. Hi uweze kunufaika na ufugaji
ni lazima uwe na mifugo bora.
Kitabu hiki kimeandikwa
ili kukupatia maarifa na mbinu za kutumia ili upate kuku bora
kutokana na kuku wako wa kienyeji.
Katika kitabu kingine “ Kufuga kuku wa biashara” Utajifunza maarifa na mbinu bora
za ufugaji wa kuku wa biashara.
Hawa ni kuku wa kigeni.
Wanahitaji matunzo maalum tofauti
na yale ya kuku wa kienyeji wanaoboreshwa.