Kwa ufupi:
TANU ya sasa ina kazi kubwa sana, maana TANU
inafanya kazi ya kuelimisha, kueleza na kujcnga Taifa letu ili
litoke katika hali ya unyongc na kuwa katika hali ya neema na
nguvu. Kania sote tunavyoelcwa ni kwamba katika kuwaongoza
wananchi. ni budi kwanza tuwasikilize, tushirikiane nao na
tufanye kazi pamoja nao. Uhusiano uliopo kati ya Serikali na
chama cha TANU ni mkubwa. J ambo la kukumbukwa ni
kwamba chama siyo chombo cha Serikali, bali ni Serikali
ambayo ndiyo chombo kinachotumiwa na chama katika
kutekeleza matakwa yo vote ya wananchi ambao sisi sote
tunawatumikia. Hii ndiyo maana tunasema kuwa chama kina
wajibu mkubwa wa kufanya, katika kufikiria misingi ambayo
baada ya kuwekwa kwa uwazi, ni budi Serikali ifuate na
kutekeleza. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ni sehemu
ya Serikali. Hivyo Wizara hii ina wajibu mkubwa sana katika
kuitekeleza siasa ya TANU ambayo ndiyo inayoongoza Serikali.