Kwa ufupi:
Kabla ya Tanzania kupata uhuru, serikaii ya kikoloni ilijiingiza
sana katika mazao ya biashara na nchi za nje na haikujali sanajuu
ya mazao yaliyotumika humu nchini hasa yale ya chakula ambayo
wananchi hutumia. Siasa yao ya kikoloni wakati huo ilikuwa kuku-
za mazao ambayo yangeuzwa na kukuza uchumi wa nchi zao.
Siasa hiyo kwa kweli iliweza kuleta madhara kwa mazao ambayo yangetumika au kuliwa humu nchini, kwa hiyo upanuzi wa kilimo cha mazao machache kuliifanya Tanganyika kutesemea mazao kama katani na kahawa kuwa mazao makuu ya biashara na nchi za nje.