Kwa ufupi:
Kaya zinazojihusisha na kilimo zinahitaji sera wezeshi za umma ili ziweze kuendana na kustawi katika mazingira ya sasa yanayobadilika kila uchao, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva.
Akizungumza mjini New York, Marekani wakati wa uzinduzi wa muongo wa Umoja wa Mataifa wa kilimo cha kaya kando mwa jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu
maendeleo endelevu, HLPF, Bwana da Silva amesema “tunahitaji kurekebisha mifumo yetu ya chakula na kuihusisha na shughuli za muongo wa kilimo cha kaya sambamba na muongo wa hatua za kuimarisha lishe.”