Kwa ufupi:
Kitabu hiki cha “Uzalishaji bora wa mbuzi wa nyama" kimetayarishwa na mtaalam na muelimishaji wa somo la mbuzi na kondoo kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kwa Aiidi ya miaka 35, Profesa Edith Ndcmanisho. Lengo kubwa la kitabu hiki ni kuwaelimisha wafugaji wadogo wadogo wa mbuzi juu ya ufugaji wa kisasa ili kuongeza pato na lishe kwa familia. Aidha, kimetayarishwa kwa kutumia lugha rahisi inayomwczesha mkulima kuelewa yaliyomo kwa urahisi. Nchini Tanzania kuna mbuzi wanaokadiriwa kufikia milioni 24.5. Hadi
sasa. kuna miradi michachc ya utafiti na macndclco ya uzalishaji wa wanyama hawa. Wafugaji wa inbuzi hawajaelimishwa juu ya mbinu mbali mbali za uzalishaji. Kwa hiyo kuna matatizo mengi yanayoathiri shughuli za uzalishaji wa mbuzi ikiwa ni painoja na ulishaji bora, uzalishaji (breeding), mabanda. magonjwa na utunzaji kwa ujumla. Soko la mbuzi ni kubwa hasa katika
nchi za Uarabuni na huwa wanatafuta mbuzi wa nyama kwa wingi kutoka Tanzania. Ni vyema wafugaji wa mbuzi wakachangamkia hili soko kwani majirani zetu Kenya huwa wanao mbuzi bora ila idadi yoke sio kubwa kama ya nchini Tanzania.