Kwa ufupi:
Katika kundi la mazao ya mizizi, viazi mviringo ni maarufu na vina umuhimu wa pekec. Ni zao la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizocndclca na zinazocndclea. Zao hili ni moja ya mazao manne ya chakula yanayozalishwa kwa wingi na kutumiwa na watu wengi sana duniani. Hustawi vizuri kwenye
sehemu za miinuko, kati ya meta 1,300 na 2,700 juu ya usawa wa bahari. Kipindi cha kukomaa ni kati ya miezi mitatu na mitano.Mbali na utamu wa viazi mviringo, lakini mlaji hujipatia asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Aidha, vina kiasi cha kutosha cha protini, madini, vitamini na maji.