Kwa ufupi:
Kiungo maarufu katika sehemu nyingi za dunia, giligilani ni shujaa asiyejulikana wa vyakula vya Kihindi. Na sasa mpishi mmoja anataka kukifufua, akiipa giligilani "utukufu unaostahili".
Ukichunguza ndani ya viboksi vyovyote vya viungo vya Kihindi, kuna uwezekano mkubwa kukuta viungo - manjano, pilipili nyekundu ya unga na giligilani ya kusaga (mara nyingi vikichanganywa na binzari) - ambayo ni msingi wa vyakula vingi vya mboga. Ingawa haina rangi ya kuvutia kama manjano na haihusiani na ladha yoyote ya viungo vya India, giligilani (inayojulikana sana dhaniya au kothmir nchini India) labda ndiyo inayotumika zaidi kati ya viungo hivi vingi.
Mbegu zake zilizosagwa huongeza ladha kwenye vyakula vingi, wakati unga wake, unaweza kutumika kutengeneza Curry Powder. Mmea wake mabua na majani yake mbichi mara nyingi hutumika kama ladha ya kumalizia yenye harufu nzuri na tamu.