Kwa ufupi:
Kitabu hiki kitaangazia sehemu ya hapo awali, ili kutoa maelezo kuhusu kuambatanisha miti na mimea mingine katika kuimarisha mazao na kuendeleza uhai-anuai. Ni muhimu kufahamu kwamba hakuna njia moja ya kuimarisha na kufanikisha kilimo, bali mbinu za kila aina zapaswa kutekelezwa. Mbinu hizi zaweza kujumuisha jamii nzima katika kupanda miti ya kienyeji, miti mingine yenye manufaa, mbinu za kutunza udongo na njia nyinginezo za kuimarisha kilimo cha mseto. Kilimo cha mseto hunufaisha sehemu kame, zile zisizotumika kwa kikamilifu au hata zile za tindikali au udongo wa chumvi nyingi.