Kwa ufupi:
Mwongozo huu umeandaliwa ili kusaidia jamii na watunga sera katika ngazi ya jamii na kitaifa kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi kuhusu matumizi ya ardhi, biashara, na sera za kitaifa kwa maeneo ya wafugaji, hasa nyika za umasaini na maeneo makame ya Afrika ya Mashariki. Kitini hiki kinachoeleza mfumo wa kusaidia ufanyaji maamuzi, Kudumisha uhusiano kati ya jamii, ufugaji na wanyamapori ni matokeo ya kazi iliyofanywa na Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori Afrika (AWF) na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mradi wa Mifumo mipya ya kujumuisha mifugo na wanyamapori kwenye maeneo ya malisho yaliyopo pembezoni mwa hifadhi za Taifa katika Afrika - Tanzania uliofadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) na Benki ya Dunia.