Kwa ufupi:
Zao la karafuu ni kiungo maarufu kinachotumika duniani kote. Asili ya Zao la mkarafuu ni
Indonesia, India, Pakistan na hata maeneo ya nchi za Afrika Mashariki kama Zanzibar. Maeneo
mengine ya Tanzania yanayoweza kulima zao la karafuu ni pamoja na mikoa ya Morogoro na
Tanga.
Zao la karafuu lilipelekwa visiwa vya Unguja na Pemba na kuanzisha uzalishaji wa zao la
karafuu kwenye visiwa hivi na mtawala wa Omani.
Uzalishaji wa zao la karafuu katika visiwa vya Zanzibar umekuwa ukiongezeka mwaka hadi
mwaka na kufikia tani 3, 5000 kwa na kufikia soko la karafuu duniani kwa asilimia 90.
Zao la karafuu hustawi katika nyuzi joto 26.1-26.7°C na kukua vizuri kwenye sehemu yenye
mwinuko wa usawa wa bahari m. 800-900 na ili zao hili liweze kustawi na kukua vizuri linahitaji
mvua yenye wastani wa mm. 1628 mpaka mm. 1963 kwa mwaka