xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | Wizara ya Kilimo | |
dc.date.accessioned | 2023-10-05T10:12:52Z | |
dc.date.available | 2023-10-05T10:12:52Z | |
dc.date.issued | 2012-10 | |
dc.identifier.issn | 1821 - 8113 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/755 | |
dc.description.abstract | Ndugu wakulima; sote tunaelewa kwamba ili kupata chakula kilicho bora na cha kutosha mbinu mchanganyiko na mikakati ya utumiaji mzuri wa mbolea unahitajika. Njia hii inamsaidia mkulima kurutubisha ardhi na kupata mazao mengi na yaliyo bora kutokana na matumizi ya mbolea za mboji, samadi za wanyama na za viwandani. Ndugu wakulima; mimea ni kama binadamu inahitaji lishe nzuri na ili mimea iwe yenye afya. Lishe hiyo hupatikana kwa matumizi bora ya mbolea hizo tulizozitaja na pindipo ikikosekana mimea hudumaa, majani huwa na rangi ya kijani kibichi kilicho fifia na kushindwa kutengeneza chakula ipasavyo hatimae mazao hupungua shambani. Ndugu wakulima; ili mavuno yaweze kuongezeka na kuwa bora wakulima wanapaswa kufuata kikamilifu kanuni za kilimo bora. Moja kati ya kanuni hizo ni matumizi ya mbolea yanayozingatia utumiaji, muda mzuri unaofaa kuweka mbolea na kufahamu mahitaji halisi pamoja na kiwango kinachohitajika kwa kila eneo pamoja na aina ya mbolea. Ndugu wakulima; matumizi ya mbolea hupelekea mimea kustawi kwa haraka na kuongeza mavuno mara dufu. Mbolea inapotumika vizuri mazao hupatikana kwa gharama ndogo ambapo uwezo wa asili wa udongo kutoa mazao kutegemea rutuba huwa mkubwa. Ndugu wakulima; ni vizuri tufahamu kuwa matumizi bora ya mbolea ni muhimu sana ambapo inaaminika kuwa matumizi ya hayo peke yake huongeza mazao kwa asilimia 50 kama takwimu zinavyoonesha na humsaidia mkulima kupata fedha za kulipia gharama nyingine zitakazotumika kwa kufuata kanuni za kilimo bora ikiwemo kutumia mbegu bora, madawa ya kuzuwia wadudu, magonjwa, kupanda kwa wakati kuongeza mazao kwa asilimia 50 iliyobakia. Ndugu wakulima; kwa kuzingatia matokeo muhimu ya uzalishaji matumizi ya mbolea yatapungua iwapo vipo vitu vyengine vitakavyopunguza mavuno ya mazao, kwa mfano magugu yanaokwamisha ukuaji mzuri wa mazao. Hivyo, faida ya matumizi ya mbolea hugeuka na kuwa hasara ikiwa mbolea hiyo itawekwa katika shamba lenye magugu, kwa sababu gugu likipata mbolea hupata nguvu na kufanya mimea kunyong’onyea. Ndugu wakulima; ili kufanikisha mpango wa taifa wa kujitosheleza kwa chakula Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili inaendeleza juhudi za kuwasaidia na kuwahamasisha wakulima wazidi kujitokeza kwa wingi katika kutumia mbolea | en_US |
dc.publisher | Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar | en_US |
dc.relation.ispartofseries | ;12 | |
dc.subject | Utunzaji Miti | en_US |
dc.subject | Utunzaji Mazingira | en_US |
dc.subject | Ufugaji | en_US |
dc.subject | Mbuzi | en_US |
dc.subject | Kondoo | en_US |
dc.title | Utunzaji wa Miti | en_US |
dc.type | Article | en_US |