Kwa ufupi:
Ndugu wakulima; sote tunaelewa kwamba ili kupata chakula kilicho
bora na cha kutosha mbinu mchanganyiko na mikakati ya utumiaji
mzuri wa mbolea unahitajika. Njia hii inamsaidia mkulima kurutubisha
ardhi na kupata mazao mengi na yaliyo bora kutokana na matumizi ya
mbolea za mboji, samadi za wanyama na za viwandani.
Ndugu wakulima; mimea ni kama binadamu inahitaji lishe nzuri na
ili mimea iwe yenye afya. Lishe hiyo hupatikana kwa matumizi bora
ya mbolea hizo tulizozitaja na pindipo ikikosekana mimea hudumaa,
majani huwa na rangi ya kijani kibichi kilicho fifia na kushindwa
kutengeneza chakula ipasavyo hatimae mazao hupungua shambani.
Ndugu wakulima; ili mavuno yaweze kuongezeka na kuwa bora
wakulima wanapaswa kufuata kikamilifu kanuni za kilimo bora. Moja
kati ya kanuni hizo ni matumizi ya mbolea yanayozingatia utumiaji,
muda mzuri unaofaa kuweka mbolea na kufahamu mahitaji halisi
pamoja na kiwango kinachohitajika kwa kila eneo pamoja na aina ya
mbolea.
Ndugu wakulima; matumizi ya mbolea hupelekea mimea kustawi kwa
haraka na kuongeza mavuno mara dufu. Mbolea inapotumika vizuri
mazao hupatikana kwa gharama ndogo ambapo uwezo wa asili wa
udongo kutoa mazao kutegemea rutuba huwa mkubwa.
Ndugu wakulima; ni vizuri tufahamu kuwa matumizi bora ya mbolea
ni muhimu sana ambapo inaaminika kuwa matumizi ya hayo peke
yake huongeza mazao kwa asilimia 50 kama takwimu zinavyoonesha
na humsaidia mkulima kupata fedha za kulipia gharama nyingine
zitakazotumika kwa kufuata kanuni za kilimo bora ikiwemo kutumia
mbegu bora, madawa ya kuzuwia wadudu, magonjwa, kupanda kwa
wakati kuongeza mazao kwa asilimia 50 iliyobakia.
Ndugu wakulima; kwa kuzingatia matokeo muhimu ya uzalishaji matumizi
ya mbolea yatapungua iwapo vipo vitu vyengine vitakavyopunguza
mavuno ya mazao, kwa mfano magugu yanaokwamisha ukuaji mzuri
wa mazao. Hivyo, faida ya matumizi ya mbolea hugeuka na kuwa hasara
ikiwa mbolea hiyo itawekwa katika shamba lenye magugu, kwa sababu
gugu likipata mbolea hupata nguvu na kufanya mimea kunyong’onyea.
Ndugu wakulima; ili kufanikisha mpango wa taifa wa kujitosheleza kwa
chakula Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo
na Maliasili inaendeleza juhudi za kuwasaidia na kuwahamasisha
wakulima wazidi kujitokeza kwa wingi katika kutumia mbolea