Kwa ufupi:
Kabla ya jamii kushirikishwa
katika uhifadhi wa maliasili
misitu eneo la Jozani na
ghuba ya chwaka, Ndugu Simai
alieleza kwamba Serikali pekee
ndio iliyokuwa ikilinda rasilimali
hizo zilizozungukwa na vijiji tisa
vyenye wakaazi wasiopungua
42, 000. Ilionekana kwamba
mwananchi wa kawaida kama
ni adui wa maliasili japokuwa
ndio mwenye mahitaji makuu
ya kutumia maliasili hizo kwa
maisha ya kila siku. Mwananchi
alijenga dhana kwamba maliasili
za misitu ni za Serikali na wao
hawana mamlaka ya kufaidika
na hilo na kupelekea kuwepo na
mvutano baina ya mwananchi
na Serikali katika matumizi
ya maliasili na kusababisha
uharibifu katika matumizi.
Baada ya Serikali kutanabahi
kwamba haitamudu kazi ya
uhifadhi kwa ufanisi, wakati
uharibifu wa maliasili za misitu
unaongezeka na mvutano
baina ya Serikali na wananchi
unaongezeka, Idara ya Misitu
ilitoa wazo la kushirikisha jamii
katika uhifadhi wa maliasili za
misitu ili iwe na hisia kwamba
rasilimali zilizowazunguka ni
zao na wanahusika katika
jukumu la uhifadhi. Mnamo
mwaka 1996 likatolewa wazo la
kuanzisha Kamati za Uhifadhi.
Kamati saba za kusimamia
matumizi ya maliasili
zilianzishwa katika Shehia za
Pete (Jozani), Unguja Ukuu,
Cheju, Chwaka, Charawe,
Ukongoroni na Bwejuu. Baadae
iliundwa Kamati ya ushauri
baina ya Idara ya Misitu na
kuwashirikisha wajumbe wawili
kutoka kila kamati ambapo kazi
za uhifadhi zikiratibiwa na mradi
wa kimataifa wa CARE. Kamati
hiyo ya ushauri ilifanya kazi kwa
pamoja ambapo Idara ilitoa
wazo la kuundwa kwa Jumuiya
ya Uhifadhi wa Mazingira Jozani
(JECA) kwa lengo la kuendelea
na kazi za uhifadhi baada ya
mradi wa CARE