xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | Wizara ya Kilimo | |
dc.date.accessioned | 2023-10-05T09:57:51Z | |
dc.date.available | 2023-10-05T09:57:51Z | |
dc.date.issued | 2013-10 | |
dc.identifier.issn | ISSN: 1821 - 8113 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/753 | |
dc.description.abstract | Ndugu wakulima, kupata chakula cha kutosha na kilicho bora kwa kila mwananchi ni suala gumu ambalo linahitaji mipango na mikakati mizuri ya serikali kupitia Wizara husika. Matatizo makubwa yanayowakabili wananchi ni kuchelewa kukamilisha hatua za mwanzo za matayarisho ya mashamba, kulima eneo kubwa ambalo hawana uwezo nalo na kutokutumia njia za utaalamu pamoja na pembejeo bora za kilimo. Ndugu wakulima, moja ya kikwazo kikubwa ni uwezo mdogo wa kutumia zana bora za kilimo, mbegu bora, mbolea na kutozingatia kanuni na taaluma bora za uzalishaji ambazo zinatolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili. Vikwazo hivi humsababishia mkulima kutumia nguvu nyingi, muda mrefu na kupata mavuno hafifu na tija ndogo. Ndugu wakulima, kwa miaka mingi neno “Ukulima wa Kisasa” limekuwa ni wimbo lakini bado mkulima wa visiwani anategemea zana na pembejeo duni kama vile mbegu na jembe la mkono (kijembe kongoroka). Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili inafanya mabadiliko makubwa katika kilimo ili kukifanya kilimo hicho kiwe katika mfumo wa kisasa “Mapinduzi ya Kilimo”. Ndugu wakulima, katika kufanikisha suala hili Serikali imeongeza upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo yakiwemo matrekta makubwa na madogo, mbegu bora na mbolea, kuongeza usamabazaji wa taaluma kwa wakulima kwa kuongeza idadi ya mabwana/ mabibishamba katika shehia pamoja na kutoa ruzuku ya aslimia 75% kwa kazi za utayarishaji wa mashamba na ununuzi wa mbegu bora na mbolea. Ndugu wakulima, hatunabudi kuunga mkono juhudi hizi za Serikali ili kufanikisha azma ya “Mapinduzi ya Kilimo” hivyo tunaipongeza na tunaiomba iendelee na juhudi zake za kuwashajiisha na kuwashirikisha wakulima kikamilifu katika kupanga malengo yao juu ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini. Ndugu wakulima, kwa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali, Wizara ya Kilimo na Maliasili itaendelea kutoa mafunzo ya utumiaji bora wa zana na pembejeo za kilimo na kuweka mipango maalumu ya mafunzo kwa kila shehia juu ya umuhimu wa zana hizo pamoja na matumizi yake ili kufikia lengo la wakulima katika kujitosheleza kwa chakula na kuimarisha afya za jamii pamoja na kuinua hali zao za maisha na kuipunguzia mzigo Serikali kwa kuagiza chakula kutoka nje ya nchi | en_US |
dc.publisher | Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar | en_US |
dc.relation.ispartofseries | ;10 | |
dc.subject | Tugule | en_US |
dc.subject | Mbuzi | en_US |
dc.subject | Kondoo | en_US |
dc.subject | Uyoga | en_US |
dc.title | Kilimo cha Tungule | en_US |
dc.type | Article | en_US |