Kwa ufupi:
Pilipili hoho kama linavyotambulika kitaalamCapsicum annuumni zao la mboga mboga lenye asili ya Amerika ya Kusini ambako lilisambaa mpaka sasa kulimwa katika maeneo mengi duniani yenyehali ya hewatofauti.Hapa Tanzania pilipili hoho hulimwa kwawingi katika mikoa ya Morogoro (Mgeta, Mlali) Arusha, Iringa, Kilimanjaro na Mbeya. Sehemu nyingine zinazolima pilipili hoho ni Ruvuma na Tabora. Pilipili hoho huzaa matunda ya rangi tofauti kama vile kijani, nyekundu, njano, machungwa na zambalau. Kwa Tanzania pilipili zinazolimwa kwa wingi ni zile za matunda ya kijani, nyekundu na njano