Kwa ufupi:
Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi.
Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika
kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro
na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi,
mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile
maharage.
Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo
litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni
pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi
zinazotambulika katika masoko ya kimataifa.