Kwa ufupi:
Kitabu hiki, “Uzalishaji Bora wa Kondoo wa Nyama” kimetayarishwa na mtaalam na mfundishaji
wa somo la mbuzi na kondoo kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (kwa zaidi ya miaka
35), Profesa Edith Ndemanisho. Lengo kubwa la kitabu hiki ni kuwaelimisha wafugaji wadogo
wadogo wa kondoo juu ya ufugaji wa kisasa ili kuongeza pato na lishe kwa familia. Aidha,
kimetayarishwa kwa kutumia lugha rahisi inayomwezesha mkulima kuelewa yaliyomo kwa urahisi.
Nchini Tanzania kuna kondoo wanaokadiriwa kufikia milioni 6.0. Hadi sasa, kuna miradi michache
sana ya utafiti na maendeleo ya uzalishaji wa wanyama hawa. Wafugaji wa kondoo
hawajaelimishwa juu ya mbinu mbali mbali za uzalishaji. Kwa hiyo kuna matatizo mengi
yanayoathiri shughuli za uzalishaji wa kondoo ikiwa ni pamoja na ulishaji bora, uzalishaji
(breeding), mabanda, magonjwa na utunzaji kwa ujumla. Soko la kondoo ni kubwa hasa katika nchi
za Uarabuni na huwa wanatafuta kondoo kwa wingi kutoka Tanzania. Ni vyema wafugaji wa
kondoo wakachangamkia hili soko kwani majirani zetu Kenya huwa wanao kondoo bora ila idadi
yake sio kubwa kama ya nchini Tanzania.
Kondoo wa nyama wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu
kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza
kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvu kazi na kipato
kidogo. Uzao wao ni wa muda mfupi (anabeba mimba miezi mitano tu) unamwezesha mfugaji
kupata kondoo wengi kwa kipindi kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa,
ngozi, mbolea, sufu na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.
Kitabu hiki kinaeleza mbinu mbali mbali juu ya utunzaji bora wa kondoo na kimegawanywa katika
sura kuu sita ambazo ni Hali ya sasa ya ufu