Kwa ufupi:
Kaa ni kiumbe anayeishi kwenye
mchanganyiko wa maji bahari na maji baridi.
Jamii ya kaa anayefugwa kwa wingi hapa
nchini anajulikana kama kaa-ungo na kitaalam
hujulikana kama Scylla serrata (mud crab au
mangrove crab). Kaa hawa huishi kwenye
mikoko na mara nyingi hujichimbia kwenye
tope. Kaa wanakua kwa kujivua gamba kila
hatua ya ukuaji. Faida za kunenepesha kaa ni
pamoja na kuongeza kuongeza uzito na ubora
wa nyama, kipato, kupunguza vifo na
kuhifadhi mazingira ya mikoko.