Kwa ufupi:
Mnyama huyu huaminika ndiye mwaminifu zaidi kati ya wanyama wote wanaofugwa nyumbani
Kuna wale wanaomfuga pia kwa sababu humchukulia kama ‘kipenzi’ chao (pet).
Je, wajua mbwa ni kitega uchumi kwa baadhi ya wanaomfuga? Mnyama huyu ametajirisha baadhi ya wafugaji wanaomthamini.
Mbwa hawa hufugwa na kutunzwa kwa msingi wa malengo matatu, wale wa kunusa (sneaver dogs), wa kulinda/kuhifadhi usalama (guard dogs) na wa kuongoza (guide dogs) maafisa wa usalama.
Mbwa huzaa mara mbili kwa mwaka ambapo hubeba ujauzito kwa kipindi cha siku 63 (miezi 2).
Kwa kawaida mbwa mmoja huzaa kati ya vilebu 8 – 12.