Kwa ufupi:
Tatizo la minyoo Tegu ya nguruwe limetajwa kuwa ni kubwa hali ambayo inawalazimu wataalamu na wanasayansi kufanya utafiti wa kina ili kupata majibu ya tatizo hilo.
Wataalamu kutoka sehemu mbalimbali duniani, wamekusanyika ili kujua jinsi ya kukabiliana na minyoo ya Tegu ya nguruwe, ambayo imedhihirishwa kitaalamu kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu, hususani kwa watumiaji wa kitoweo cha mnyama huyo, maarufu hapa nchini kama Kitimoto.
Tafiti zimeonesha kuwa, kwa mwaka mmoja Tanzania inapoteza zaidi ya shilingi bilioni 19 kutokana na athari zinazotokana na Minyoo tegu ya Nguruwe kwa jamii ikiwemo matibabu na kutupa nyama yenye maambukizi