Kwa ufupi:
Ili kuendana na Mpango wa Taifa wa
Maendeleo wa Miaka Mitano (2016 - 2021)
inayosisitiza Tanzania ya Viwanda,
inashauriwa ufugaji wa samaki ufanyike
kwa kutumia teknolojia za kisasa zenye tija
kwa ajili ya kuongeza uzalishaji. Ufugaji wa
samaki kwa kutumia mabwawa ndiyo njia
iliyozoeleka na inayotumiwa na wananchi
wengi. Hivi karibuni kumekuwepo na
ongezeko la ufugaji wa samaki kwa kutumia
vizimba katika maji ya asili. Mabadiliko haya
kwa kiasi kikubwa yametokana na
mabadiliko ya tabianchi (hususani upungufu
wa mvua), uwepo wa teknolojia ya vizimba
na wingi wa mavuno yanayotokana na
ufugaji wa samaki kwenye vizimba.