Kwa ufupi:
Mkonge ni moja kati ya zao la biashara ambalo jina lake la kisayansi linaitwa Agave sisalana.
Mikoa ambayo zao la mkonge linasitawi katika nchi ya Tanzania ni Tanga, Morogoro,
Kilimanjaro, Shinyanga, Geita, Mwanza, Mara, Pwani, Linda na Simiyu.
Mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, ukosefu wa vipando bora, magonjwa na wadudu
waharibifu yamefanya wakulima wengi wadogo kukosa mavuno ya kutosha kwa mazao
mbalimbali. Hivyo, watafiti wa zao la mkonge wanahamasisha kilimo cha mkonge kwa
wakulima wadogo nchi nzima kwa kuwa zao hili linastahimili ukame, majonjwa, wadudu,
magugu, ukame na hata upungufu wa rutuba kwenye udongo.
Mkulima anaweza kupata faaida mbalimbali kutokana na kilimo cha mkonge hususani kama
mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi kwa muda mfupi na
muda mrefu. Baadhi ya faida za kilimo cha mkonge ni kama zifuatazo:
(i) Ajira na kipato: Kilimo cha mkonge huweza kutoa ajira nzuri sana kwa familia kwani ni
zao hili halina uhaba wa vipando na bidhaa zinazotokana na zao hili zinaweza kutumika katika
sekta ya kilimo, nishati, ujenzi, famasia na ofisini. Na pia zao hili linaweza kudumu miaka
10-25 hivyo kumuhakikishia mkulima kipato cha uhakika.
(ii) Matumizi bora ya ardhi: Zao hili linaloweza kuchanganywa na mazao mengine ya
msimu kama kunde, mahindi, maharage, alizeti na karanga