Kwa ufupi:
Chakula bora cha samaki ni hitaji muhimu katika ukuaji wa samaki. Matumizi ya
chakula duni husababisha udumavu wa samaki. Kwa kawaida, bwawa
lililorutubishwa, hutengeneza chakula cha asili ambacho ni nafuu na hupunguza
gharama za uzalishaji. Ili kufuga kwa tija na kupata mavuno makubwa, inashauriwa
mfugaji atumie chakula bora cha ziada. Ubora wa chakula ni pamoja na uwepo wa
virutubisho muhimu na urahisi wa
kumenge’nywa na samaki.