Kwa ufupi:
Utafiti huu unahusika na kuboresha uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko ya nyanya Tanzania, ikichukulia wilaya mbili kama kielelezo. Wilaya hizo ni Kisarawe tarafa ya Maneromango na Msanga na Morogoro vijijini, tarafa ya
Mikese. Utafiti huu shirikishi unafanyika kati ya wakulima, watalaamu kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Morogoro na wagani wa Kilimo kutoka wilaya zilizotajwa.
Kijarida hiki kimeandaliwa ili kitumike katika kueneza mbinu mbalimbali zinazohusika na uzalishaji wa nyanya shambani. Mbinu hizi ni pamoja na kuchagua aina nzuri ya nyanya, matayarisho ya kitalu, utunzaji wa nyanya shambani na hatimaye uvunaji.