Kwa ufupi:
Hakuna kitakachorekebisha ubora wa maziwa yakiwa yamesha haribika kwa mfugaji. Kwahiyo utunzaji wa maziwa, usafi na kudhibiti ubora hauna budi kuzingatiwa katika hatua zote za mlolongo wa thamani ya maziwa. Uzalishaji wa maziwa yenye ubora wa hali ya juu huanzia sehemu ya kukamulia, ambayo lazima iwe safi , kavu na yenye hewa ya kutosha. Ngombe anatakiwa kukamuliwa kwenye sakafu laini isiyoteleza (saruji ikiwezekana). Sakafu hii inatakiwa iwe na mteremko kidogo ili kutiririsha majimaji na taka nyingine..