Kwa ufupi:
Kwa karne nyingi wafugaji wamekuwa wakimudu mifugo yao na nyanda za malisho kwa kuhamahama kufuatana na majira, wakitunza maeneo ya malisho kwa msimu wa kiangazi, wakihifadhi aina fulani fulani za miti, na kujiepusha na maeneo yajulikanayo kuwa na maradhi. Utaratibu huu wa kimila wa mpango wa matumizi ya ardhi ulisaidia mifugo na wanyamapori kusitawi vizuri kwenye nyika za Umasaini, ambazo hadi sasa zina idadi kubwa ya mamalia wakubwa ulimwenguni. Lakini katika miongo ya karibuni sera za serikali na kukua kwa ongezeko la watu vimesababisha kupungua kwa uhuru wa kuhamahama kwa wafugaji, ukiibana mifugo kwenye maeneo yenye nafasi ndogo.