Kwa ufupi:
Moja ya matarajio makubwa ya mradi huu wa AVA ni kusadia jamii kuibua miradi ya maendeleo mbayo ni rafiki wa misitu na mazingira. Hivyo mojawapo ya miradi iliyoibuliwa na wanakijiji wa Halmashauri ya Mvomero, Morogoro ni ufugaji wa kuku wa asili. Baada ya kuonekana fursa iliyopo katika kuondoa umasikini na kuongeza kipato cha wananchi, mradi ulifanya zoezi la kutambua kaya masikini na hivyo kuamua kuzipatia mafunzo juu ya ufugaji kuku wa asili.