Kwa ufupi:
Muhogo ni zao lenye uwezo wa kustahimili ukame hivyo linaweza kulimwa hat
sehemu zenye mvua chache. Hustawi vizuri zaidi katika sehemu zenye joto. Sehemu
za baridi zao hili juchelewa sana kukomaa na pengine kushindwa kabisa kustawi.
Muhogo huhitaji udongo tifutifu au wa kichanga kiasi na wenye rutuba ya wastani.
Udongo mzito unaotuamisha maji haufai kwa kilimo cha muhogo. Muhogo licha ya
kuwa chakula cha binadamu, una matumizi mengi. Majnai yake machanga hutumika
kama mboga ijulikanayo kwa jina la kimsamvu. Majani haya yana vitamini A kwa
wingi.