Napenda kuwaletea somo la jinsi ya
kulea vifaranga vya kuku, hivyo usiache kua nasi ili kujifunza mengi zaidi.
Na tutaanza na jinsi ya kujenga nyumba ya vifaranga, hivyo ukitaka kujenga nyumba ya vifaranga
ni lazima uzingatie yafuatayo.
Nyumba ya vifaranga nilazima ijengwe karibu na nyumba ya muangalizi hii ni kwaajiri ya
kuweza kuwa karibu kwa uangalizi zaidi.
Nyumba ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa hii nikwaajili ya
kupunguza maambukizi ya magonjwa.
Nyumba ya vifaranga isiruhusu unyevu, baridi na wanyama au wadudu kuingia ndani, lakini
ni lazima iwe na mwanga wakutosha
Pia nyumba ya vifaranga inatakiwa kua na uwazi wa kutosha kuwezesha vifaranga
kutobanana na waweze kutembea kwa uhuru.
pia ijengwe eneo ambalo haliruhusu upepo kutoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa
kuingia hii itapunguza maambukizi ya magonjwa.