Kwa ufupi:
Napenda kukuletea somo kuhusu kilimo cha Muhogo. Kama kawaida kazi yangu kubwa ni
kuhakikisha unafanikiwa kwenye eneo la kilimo, kwa kukuletea elimu sahihi na fursa mbalimbali
zinazohisiana na Kilimo. Wiki iliyopita tuliangazia kwa kifupi fursa ya kilimo cha Papai. Leo
nitapenda tuangazie fursa ya kilimo cha Mihogo.
Je wajua China na Tanzania zimesaini Mkataba wa
Soko la Mihogo? Kama hufamu basi nikuelezee kwa
ufupi. Ni hivi, Nchi ya China ni moja ya nchi
zinazotumia sana zao la muhogo. China imeingia
mkataba na Serikali ya Tanzania wa soko la mihogo,
ambapo Tanzania itapaswa kuuza China mhogo Tani
laki moja (100,000) kwa mwaka. Hata hivyo toka
mkataba huo usainiwe hadi leo mwaka mmoja tayari
umepita. Ila kwa mwaka wa kwanza, Tanzania
tulifanikiwa kuuza tani 10,000 pekee (sawa na
asilimi 10% tu ya kiasi kinachohitajika). Hivi karibuni nilimsikia Balazi wa China nchini Tanzania,
Wang Ke akisema, licha ya kuingia makubaliano na Tanzania ya kununua tani 100,000 za mihogo
kwa mwaka, kwa sasa wanapata tani 10,000 pekee. Pia akashauri kuwepo kwa ushirikiano baina ya
serikali, sekta binafsi na wakulima ili mihogo mingi izalishwe.