Kwa ufupi:
FAIDA ZA KUFUGA KAMBARE
• Kambare ni aina ya samaki wanaoweza kukua hadi kufi kia kilo 10 na hivyo humuwezesha
mfugaji kujipatia kipato na nyama zaidi kuliko perege na aina nyingine za samaki.
• Nyama ya kambare imethibitishwa kuwa na kirutubisho kijulikanacho kama Omega-3, ambacho
humpunguzia mlaji uwezekano wa kupata athari za magonjwa mbalimbali kama vile saratani,
shinikizo la damu, na magonjwa ya akili.
− Kambare wanapofugwa pamoja na perege (kambare mmoja kwa kila perege wanne mpaka
watano), hudhibiti mazaliano ya perege, hivyo kuwawezesha kukua hadi kufikia uzito mkubwa
(mpaka kilo 5).