Kwa ufupi:
Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora,
Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na
biashara.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
Kuchagua aina bora ya mbegu
• Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango
kikubwa cha mafuta.
• Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.