Kwa ufupi:
Alizeti hutambulika kitaalamu kama Helianthus Annus na hulimwa kwa wingi karibu
maeneo yote nchini Tanzania katika nyanda za kaskazini, kati, mashariki pamoja na
nyanda za juu kusini hasa katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa,
Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara na Rukwa. Hii inatokana na
uwezo wa alizeti kustawi vizuri katika mazingira mengi tofauti bila ya kuwa na
utofauti mkubwa katika uzalishaji wake.
Asili ya zao hili ni nchini Marekani ambako lilienea katika maeneo ya Ulaya na
baadae kusambaa sehemu nyingine za dunia ambapo kwa sasa Tanzania ni nchi ya
pili Afrika kwa uzalishaji wa alizeti nyuma ya Afrika ya kusini.