Kwa ufupi:
Kuna usemi flani unatumiwa na watu wengi sana. unasema; “kazi ndio msingi wa maendeleo ya mtu yeyote” . Hata
mimi nakubaliana na usemi huu kwani ni kweli kabisa kazi ndio msingi wa hatua yoyote ya maendeleo ya mtu yeyote chini
ya msingi mkuu ambao ni Mungu. Kinyume chake, asiyefanya kazi (ya kuajiriwa/kujiajiri) basi atabaki kuwa maskini na
mtu wa shida ya kipato, mahusiano mabaya na wanadamu wenzako, kuwa tegemezi nk. Kwa kuwa tunatamani sana
kutoka katika kongwa hili la umasikini wa kipato na hali mbaya ya maisha, tunalazimika kufanya jukumu letu kuu la
kumuomba sana Mungu ili atuwezeshe kujua na kufahamu mbinu mbalimbali kisha kujifunza na kufahamu kwa makini
tena kwa njia rahisi mno za kututoa katika hali hii ya umaskini uliokithiri.