Kwa ufupi:
Swali hili ni kubwa, na pengine zito kuliko maswali
vote ambayo mkulima amekuwa akijiuliza. Ni njia ipi
bora kutumia kupandisha mfugo? Je atumike
dume anayefugwa na mfugaji moja kwa moja au
itumike teknolojia ya Uhamilishaji? Pamoja na uhamilishaji kupewa kipaumbele duniani
kote, wafugaji wengi wa Tanzania bado wanatumia
dume moja kwa moja katika kupandisha mifugo yao.
Sababu kubwa zinazotolewa za kutumia dume moja
kwa moja ni pamoja na urahisi wa kutumia, unafuu wa
gharama,
upungufu au ukosekanaji
wa huduma
hususani vifaa vya teknolojia ya uhamilishaji na pia
uelewa mdogo wa faida ya teknolojia ya uhamilishaji.