Kwa ufupi:
Silage ni chakula maalum kinachotengenezwa kwa kutumia aina yoyote ya malisho yanayofaa
kwa mifugo kama majani, nyasi, mabua ya mahindi, mtama na ufuta. Kwa kawaida silage
hutengenezwa wakati wa mvua ambapo majani hukua kwa haraka na kukatwa tena na tena
mpaka kiangazi kitakapoanza, kama una shamba binafsi la majani ya napier unaweza ukawa
unayaka kila baada ya wiki sita katika kipindi cha mvua. Silage utokea baada ya majani
kuozeshwa na vimelea katika mfumo usiotumia oxijeni (anaerobic fermentation).