Kwa ufupi:
Kwa nia ya kupambana na viashirio vya uhaba
wa chakula ambavyo zaidi husababishwa
na hali mbaya ya hewa, Serikali imekuwa
na sera ya kuzuia uuzaji wa aina kuu za vyakula
nje ya nchi. Hufanya hivyo kwa kisingizio cha
kuhakikisha taifa lina chakula cha kutosheleza
mahitaji ya wananchi wakati wote. Aidha, Serikali
inaamini kwamba vizuizi hivyo ni hatua ya kuwa
na chakula kingi nchini na kuwawezesha walaji
wamudu bei yake.
Uwepo wa vizuizi vya kusafirisha mazao nje ya
nchi na vikwazo vya kibiashara na makusudio
yake, yaliibua mijadala mikubwa.