Kwa ufupi:
Kulima bustani za uyoga ni shughuli inayotimiza kikamilifu kilimo
endelevu na zipo faida kadhaa:
? Taka na makapi ya mazao hutumika vema.
? Uzalishaji wa juu kwa kila meta mraba wa ardhi huwezekana.
? Baada ya kuvuna uyoga, makapi ya uyoga ni mbolea.
Agrodok hii inatoa maelezo kamilifu juu ya namna ya kustawisha aina
tatu za uyoga-oyster, shiitake na wood ear. Aina hizi za uyoga hasa ni
rahisi kustawishwa kwa wakulima wadogo. Kustawisha aina nyingi-
nezo za uyoga kama white button na inayotokana na nyasi za mpunga
ni utaalam tofauti sana kwa hiyo kitaandikwa kijitabu tofauti cha
Agrodok kwa aina hizo mbili za uyoga wa white button na nyasi za
mpunga.