Kwa ufupi:
Ufugaji wa kuku ni nyenzo nzuri ya kujipatia kipato katika kaya kwa sababu ufugaji wa
kuku hauhitaji mtaji mkubwa na hauna kazi kubwa kiuendeshaji. Katika ufugaji huria kuku
hujitafutia chakula wenyewe. Pia inapowezekana hupewa mabaki ya chakula, chenga,
pumba au nafaka yoyote inayopatikana katika mazingira husika. Kwa walio wengi ifikapo
nyakati za jioni, kuku hulala jikoni au ndani nyumbani kwa mfugaji mwenyewe. Ufugaji
huu ni rahisi kwa kuwa hauna gharama kubwa ila faida yake ni kitoweo tu au fedha
kidogo sana.
Kutokana na lishe duni na kuzaana wenyewe kwa wenyewe (bila kubadili jogoo), kuku
wa kienyeji walio wengi wana uzito mdogo. Wana wastani wa uzito wa robo tatu za kilo
hadi kilo moja wakiwa na umri wa zaidi ya mwaka mmoja. Ila wakitunzwa vizuri zaidi na
kuboreshwa wana uwezo wa kufikia uzito wa kilo moja hadi moja na nusu katika umri
wa miezi sita hadi nane.
Kwa upande wa utagaji wa mayai kuku wa kienyeji kwa wastani hutaga mayai 50 hadi
65 kwa mwaka. Wakitunzwa vizuri zaidi huweza kufikia uzalishaji wa mayai 80 hadi 100
kwa mwaka.
Kijitabu hiki kinatoa maelezo ya njia na kanuni mbalimbali rahisi za kuzingatia ili mfugaji
aweze kuzitumia kupata mazao mengi na bora zaidi yatakayomnufaisha kimapato na
kwa matumizi mengine. Kanuni hizi ni pamoja na:
√
Kuchagua njia bora ya kufuga na sifa za mabanda bora ya kuku
√
Kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga, kuzaliana na kutotolesha
√
Utunzaji wa vifaranga
√
Kutengeneza chakula bora cha kuku
√
Kudhibiti na kutibu magonjwa
√
Kutunza kumbukumbu
√
Kutafuta masoko