Kwa ufupi:
Lishe bora ni rnuhimu kwa watoto wote hususan wenye virusi
vya UKIMWI kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yao. Watoto
wanakua kwa haraka hivyo wana mahitaji makubwa ya chakula
ili kuwapatia virutubishi muhimu yaani nishati-lishe, protini,
madini na vitamini.
Watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wenye UKIMWI
wako katika hatari kubwa ya kupata utapiamlo kutokana na:
• Ongezeko la mahitaji ya virutubishi hasa nishati-lishe.
• Maradhi ya mara kwa mara.
• Ulaji duni.
• Uyeyushwaji na ufyonzwaji duni wa virutubishi mwilini.
Mengi ya maradhi yanayoambatana na kuishi na virusi vya
UKIMWI na UKIMWI huathiri mfumo mzima wa ulaj i wa
chakula na kusababisha lishe duni. Lishe duni hudhoofisha
mfumo wa kinga na hivyo humuweka mtoto katika hatari ya
kupata maradhi mbalimbali kwa urahisi. Maradhi na utapiamlo
kwa pamoja huhatarisha maisha ya mtoto mwenye virusi vya
UKIMWI.