Kwa ufupi:
Makala inayoelezea kwa kina juu ya Pilipili mbuzi ambalo ni zao linaloweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao
hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua (ingalau kiasi cha masaa 6 kwa siku)
Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu
ila usiwe wenye kutuamisha maji. Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni
chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefika 8 onana na
wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.