xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | Maganga, S. J. | |
dc.contributor.author | Kimboka, S. | |
dc.contributor.author | Tatala, S. | |
dc.contributor.author | Mduma, B. | |
dc.contributor.author | Ballart, A. | |
dc.contributor.author | Temalilwa, C. R. | |
dc.contributor.author | Missano, H. M. | |
dc.contributor.author | Kisanga, P. | |
dc.contributor.author | Magalia, A. W. | |
dc.contributor.author | Ng'wawasya, B. M. | |
dc.contributor.author | Kayombo, J. K. | |
dc.contributor.author | 5imonje, L. W. | |
dc.contributor.author | Ndossi, G. D. | |
dc.contributor.author | Rwebangira, C. G. | |
dc.contributor.author | Kayombo, L. C. | |
dc.contributor.author | Ntoga, B. A. | |
dc.date.accessioned | 2022-04-25T05:43:14Z | |
dc.date.available | 2022-04-25T05:43:14Z | |
dc.date.issued | 1994-10-11 | |
dc.identifier.isbn | 997691031 1 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/648 | |
dc.description.abstract | Upungufu wa wekundu wa damu ni moja ya matatizo sugu ya utaptamlo yanayoathiri watu na kusababisha vito vingi hapa Tanzania. Kutokana na takwimu zilizopo Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, inakadiriwa kuwa asilimia 32 ya watu milioni 23 (Sensa ya mwaka 1988) wanaathirika. Wanaoathirika zaidi ni wanawake wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa wanawake wajawazito wanaoathirika ni asilimia 80 na watoto chini ya umri wa miaka mitano ni asilimia 45. Tatizo la upungufu wa wekundu wa damu hutokana na sababu nyingi zikiwemo ulaji duni yaani kutokula chakula cha mchanganyiko na cha kutosheleza mahitaji ya mwili. Magonjwa mbalimbali hasa malaria na minyoo ni chanzo kimojawapo cha tatizo. Vile vile uzazi wa karibu karibu huchangia upungufu wa wekundu wa damu. Tatizo la upungufu wa wekundu wa damu hapa nchini limeenea zaidi sehemu ambazo magonjwa ya safura, malaria na kichocho hujitokeza kwa wingi. Kitabu hiki kina lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea wataalam wa ugani na viongozi katika ngazi ya wilaya, kata na kijiji ujuzi, maarifa na uwezo wa kuelewa chanzo, dalili na athari za upungufu wa wekundu wa damu katika jamii. Maarifa haya yatawawezesha kuishirikisha jamii katika kuchunguza, na kupima ukubwa wa tatizo, kufanya uchambuzi wa kina wa tatizo na kubuni mbinu za kulitatua. Kitabu kina sura tano. Sura ya kwanza inazungumzia dhana ya utapiamlo na jinsi inavyotumika katika kuchanganua tatizo la upungufu wa wekundu wa damu. Sura ya pili inaelezea umuhimu wa madini ya chuma, vitamini aina ya folic acid na B12 katika mwili wa binadamu na madhara yatokanayo na upungufu wake. Sura ya tatu inaelezea dalili na athari za upungufu wa wekundu wa damu. Sura ya nne inaelezea mbinu za kukabili tatizo la upungufu wa wekundu wa damu na sura ya tano inaelezea majukumu na wajibu wa jamii katika ngazi mbalimbali | en_US |
dc.publisher | Shirika la Chakula na Lishe Tanzania | en_US |
dc.subject | Wekundu wa damu | en_US |
dc.subject | Upungufu wa damu | en_US |
dc.title | Upungufu wa wekundu wa damu (Anaemia) | en_US |
dc.title.alternative | Kitabu kwa wafanyakazi wa ugani | en_US |
dc.type | Book | en_US |